BIMA YA MOTO / BIMA YA MAKAZI
Kama unamiliki au unakodi nyumba na vitu vilivyopo kwenye nyumba ni vya thamani, ni muhimu kuwa na bima ya moto (kwa jina lingine bima ya makazi au bima ya nyumba) ili kujipa amani ya akili na kupunguza maumivu ya kifedha ambayo utapata kwa kulipia ukarabati na kubadilisha vitu vilivyoibiwa. Wakopeshaji huwa wanawataka wakopaji wakatie nyumba zao bima ya moto kama wameweka nyumba hizo kama dhamana.
Bima ya moto kwa nyumba ya makazi (Household Insurance) ni aina ya bima inayolenga kufidia uharibifu wa nyumba, upotevu wa vifaa vilivyoko kwenye nyumba au mali ambavyo mteja ana dhamana nayo kutokana na majanga yafuatayo:
- Moto, radi na mlipuko.
- Tetemeko la ardhi.
- Milipuko ya volcano.
- Kimbunga, mafuriko.
- Kuangukiwa na mti au matawi yake.
- Kupasuka kwa mabomba makubwa.
- Kulipuka kwa matanki ya mafuta.
- Wizi au jaribio la wizi.
- Kutitia ardhi.
- Mtikisiko wa ndege au vitu viangukavyo kutoka kwenye ndege.
- Kuangukiwa na vifaa vya mawasiliano kama antenna, setelaiti, n.k.
SEHEMU A: Bima ya jengo
Inalinda nyumba dhidi ya moto na madhara mengine kama ilivyoainishwa hapo juu. Bima hii inawakinga wote, mwenye nyumba na mpangaji. Sehemu hii ya bima humpa mkataji chaguo la kuongeza majanga yanayofidiwa na bima (optional extension) kwa kuongeza malipo.
SEHEMU B: Bima ya vitu ndani ya nyumba
Inalinda vitu vilivyo ndani ya nyumba dhidi ya moto na wizi. Mfano, samani, vifaa vya muziki, televisheni, friji, n.k. Bima hii hutoa huduma hata pale mwenye bima anavyohamisha vitu vyake kwenda kwenye nyumba nyingine.
SEHEMU C: Bima ya dhima
Inamlinda mwenye nyumba au mpangaji dhidi ya hasara zitokanazo na malipo ya dhima (legal liability). Dhima hutokana na kuumia kwa mhusika wa tatu kama wafanyakazi na wageni wa kwenye nyumba, au kuharibiwa kwa mali zao kutokana na uharibifu wa nyumba au vitu vya kwenye nyumba.
Bima ya dhima humkinga mwenye nyumba au mpangaji dhidi ya:
- Matatizo kwa wafanyakazi wa ndani (dereva, mlinzi, mpishi na mtunza bustani) kama kifo, majeraha au magonjwa yaliyojitokeza wakati mfanyakazi akiwa katika majukumu yake ya kila siku.
- Mashitaka yoyote ya kisheria yanayoweza kuletwa na mfanyakazi wa ndani kutokana na ajari, magonjwa, kifo au majeraha yaliyotokea akiwa katika majukumu ya kazi.
- Kuchakaa au kushuka kwa thamani kwa nyumba au mali za kwenye nyumba.
- Uharibifu kutokana na wadudu, kuvu (fungus), kutu, au hali ya hewa.
- Uharibifu kutokana na usafishaji, marekebisho au utengenezaji wa nyumba au mali za kwenye nyumba.
- Uharibifu kutokana na ufundi mbovu.
- Uharibifu wa makusudi utakaotendwa na wanafamilia au wafanyakazi.
- Bima ya moto haitalinda wanyama ya mifugo.
- Bima ya moto haitalinda vitu vyenye bima zingine sokoni kama magari, fedha, n.k.
- Uharibifu kutokana na vita (war exclusion).
- Uharibifu kutokana na matukio yanayotumia nuklia (nuclear exclusion).
- Wauzaji wa bima wengi hulipia ghrama za huduma za zima moto.
- Vifaa vinavyohamishika ni lazima viwepo na mmliki wakati janga linatokea.
Comments
Post a Comment